u/LowSatisfaction7767

Image 1 — Vuta N'kuvute??
Image 2 — Vuta N'kuvute??
Image 3 — Vuta N'kuvute??
Image 4 — Vuta N'kuvute??

Vuta N'kuvute??

Kwa mujibu wa Google, hii ni among the best films ever made in Tanzania. Ilitoka mwaka 2021, director Amil Shivji kutoka riwaya ya Mzee Shafi Adam Shafi

Usambazaji wake umekuwa wa kimataifa sana. Ilichezwa Toronto, FESPACO, Palm Springs, Seattle, New York, Durban, Zanzibar, Carthage na Berlin. Baadhi ya watazamaji wa festival za kimataifa walipata maonyesho bure mtandaoni, kwa mfano, Cascade film festival lilifanya maonyesho 2022 bure mtandaoni. Ilishinda pia tuzo kibao, ikiwemo Tanit d'Or

Binafsi sijawai kuioona hii filamu, na nimeitafuta mnoo!! Haipo mtandaoni, haipo kwenye streaming platforms, nimeitafuta hadi piracies websites, hamna kila kitu.

Kuioona hii filamu mpaka uwe na DStv

Inakuaje filamu inayosimulia historia na utamaduni wetu iwe rahisi zaidi kuonekana kwenye film festivals nje ya nchi kuliko kwa Mtanzania wa kawaida? tunaweza kweli kusema hiyo ni success ya Tanzanian cinema?

Tatizo hapa ni filmmakers, distributors, streaming platforms, au sisi Watanzania hatuna market kubwa ya aina hii ya filamu?

u/LowSatisfaction7767 — 3 days ago

Mechi Kubwa Kuchezwa Kwa Mkapa

Hivi kwa nini hizi mechi kubwa zisichezwe Kwa mkapa? New Amaan stadium ni uwanja mzuri, lakini ni mdogo sana alafu pia ni gharama sana, hususani kwa shabiki kindakindaki anaetokea bara na anataka kucheki mechi live. Yani hapo ukihesabu nauli na kiingilio kucheki hio mechi sio chini ya laki, na hio ni Kwa anaetokea Dar, wa mkoani hapo ni gharama zaidi. Alafu pia mashabiki na wingi wao unasaidia sana katika kuongeza morali kwenye hizi mechi. Kwa mfano mi nafkiri Ile fainali ya Simba dhidi ya RS Berkane ingechezwa Kwa mkapa Simba angebeba kombe

u/LowSatisfaction7767 — 9 days ago