
Royal Norwegian Embassy in Dar es Salaam signed a NOK 7 million grant agreement with Policy Forum to strengthen transparency, citizen participation and public financial accountability in Tanzania.
Leo, Ubalozi wa Kifalme wa Norway nchini Tanzania umetia saini makubaliano ya ufadhili yenye thamani ya Krona za Norway (NOK) milioni 7 na Policy Forum kwa lengo la kuimarisha uwazi, ushiriki wa wananchi na uwajibikaji katika usimamizi wa fedha za umma nchini Tanzania.
Mradi huu wa miezi 18, utakaotekelezwa kwa ushirikiano na WAJIBU – Institute of Public Accountability, utasaidia jamii katika mikoa ya Morogoro na Mtwara kupata na kutumia taarifa za fedha za umma, kuimarisha usimamizi unaoongozwa na wananchi, na kukuza taasisi za umma zilizo wazi zaidi na zinazowajibika.
Taasisi imara na wananchi wenye taarifa sahihi ni msingi wa utawala unaowajibika na utoaji bora wa huduma za umma. Norway inajivunia kushirikiana na asasi za kiraia nchini Tanzania katika kuendeleza uwazi, uwajibikaji na maendeleo jumuishi.
———————————————————-
Today, the Royal Norwegian Embassy in Dar es Salaam signed a NOK 7 million grant agreement with Policy Forum to strengthen transparency, citizen participation and public financial accountability in Tanzania.
Implemented in partnership with WAJIBU – Institute of Public Accountability, the 18 months project will support communities in Morogoro and Mtwara to access and use public financial information, strengthen citizen-led oversight, and promote more transparent and accountable public institutions.
Strong institutions and informed citizens are essential for accountable governance and better public service delivery. Norway is proud to partner with Tanzanian civil society to advance transparency and inclusive development.
#NorwayInTanzania #GoodGovernance #Transparency #Accountability #CitizenParticipation PublicFinance Partnership SDG16